Maambukizi ya corona yapungua kwa asilimia 17

WHO yatangaza kupungua kwa kesi za maambukizi ya Covid-19 kwa asilimia 17 kote ulimwenguni

1583915
Maambukizi ya corona yapungua kwa asilimia 17

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilitangaza kuwa kumekuwa na upunguaji wa kesi za maambukizi ya corona (Covid-19) kwa asilimia 17 katika wiki iliyopita ndani ya maeneo 6 tofauti kote ulimwenguni.

Kulingana na takwimu zilizochapishwa na WHO, idadi ya kesi za maambukizi imekuwa ikipungua kwa wiki 4.

Kesi mpya milioni 3.15 za maambukizi zilirekodiwa wiki ya mwisho, ikionyesha kupungua kwa asilimia 17 ikilinganishwa na wiki iliyopita.

Upungufu wa kesi mpya zilizorekodiwa ulikuwa ni asilimia 25 Uingereza, asilimia 20 Marekani na asilimia 10 Brazil, ambazo ziliathiriwa sana na janga hilo.

Daktari wa magonjwa Jean-Marie Milleliri alisema kwamba hatua kali zilizotekelezwa mwishoni mwa mwaka wa 2020 zinaanza kuonyesha matokeo mazuri. Kulingana na Milleliri, hali ya kushuka kwa kesi inaashiria uelewa wa jinsi ya kudhibiti maambukizi ya virusi.

"Kwa kweli sio habari mbaya, lakini bado hatujui ni nzuri kwa kiasi gani," alisema Jonathan Stoye kutoka Taasisi ya Francis Crick nchini Uingereza.

Stoye alisisitiza kuwa takwimu za WHO zinaweza kukosa kuonyesha kesi kamili kote ulimwenguni kwa sababu ya data zisizokuwa wazi.

Walakini, kuna wasiwasi kwamba kuibuka kwa aina mpya ya virusi vya Covid-19 vinavyobadilika kutaathiri vibaya mwelekeo wa janga hilo.

Vile vile imetangazwa kuwa aina hii mpya ya virusi vilivyoonekana kwa uchache, vinaweza kuambukizwa kwa kasi kubwa.

Taarifa hii pia iliibua hali ya wasiwasi kwamba chanjo za virusi vya corona zinaweza kuwa na ufanisi mdogo.Habari Zinazohusiana