Makabiliano ya jeshi dhidi ya waandamanaji Myanmar

Jeshi la mapinduzi latumia risasi za plastiki kukabiliana na waandamanaji nchini Myanmar

1583974
Makabiliano ya jeshi dhidi ya waandamanaji Myanmar

Watu 4 wameripotiwa kujeruhiwa wakati wa makabiliano ya jeshi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakiendeleza maandamano ya kupinga mapinduzi ya kijeshi na kukamatwa kwa viongozi halali wa serikali nchini Myanmar.

Katika video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii na waandamanaji, jeshi la Myanmar lilionekana likitumia nguvu kukabiliana na waandamanaji na kuwalenga kwa risasi za plastiki katika jiji la Myitkyina nchini humo.

Katika taarifa iliyotolewa na vikundi vya waandamanaji, iliarifiwa kuwa watu 4 walijeruhiwa kutokana na makabiliano ya jeshi na wanahabari 5 ambao walishiriki maandamano hayo pia waliwekwa kizuizini.

Baada ya bunge kufutiliwa mbali kufuatia mapinduzi ya Februari 1, kikundi kimoja cha wabunge kilitangaza taarifa ya pamoja na kutoa wito kwa waandamanaji "kuendelea kupinga mapinduzi."

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na wanachama 15 wa chama tawala na kuchapishwa kwenye tovuti ya Myanmar Now, iliandikwa,

"Harakati za utawala wa jeshi zinalenga kukiuka haki za raia na kusimamisha mchakato wa mpito wa kidemokrasia."Habari Zinazohusiana