Jeshi lafunga Facebook nchini Myanmar

Jeshi lachukuwa uamuzi wa kufunga mtandao wa kijamii wa Facebook nchini Myanmar

1577485
Jeshi lafunga Facebook nchini Myanmar

Jeshi ambalo lilichukua madaraka kufuatia madai ya udanganyifu katika uchaguzi mkuu wa tarehe 8 Novemba 2020 nchini Myanmar, limechukuwa uamuzi wa kufunga mtandao wa kijamii wa Facebook kwa muda.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mawasiliano na Habari ya Myanmar, ilitangazwa kuwa kampuni inayomilikiwa na serikali ya MPT na viunganishi vya mtandao ya kibinafsi nchini ziliamriwa kuzuia upatikanaji wa Facebook hadi Februari 7.

Taarifa hiyo ya Wizara pia ilieleza kuchukuwa uamuzi huo ili kuhakikisha utulivu nchini, na kusema,

"Kwa sasa kumekuwa na watu ambao wanasababisha upotoshaji mbele za macho ya umma kwa kuchapisha taarifa za habari bandia kwenye Facebook."

Kufuatia maagizo ya serikali, MPT, ambayo ina watumiaji milioni 23, ilipiga marufuku matumizi ya Facebook, Instagram na WhatsApp, wakati kampuni zingine za mawasiliano zilizuia Facebook pekee.

Msemaji wa Facebook Andy Stone pia alithibitisha kuwa tovuti hiyo haikuweza kupatikana nchini Myanmar.Habari Zinazohusiana