Mauaji ya genge la watoto nchini Ufaransa

Mtoto mmoja auawa baada ya kupigwa na genge la watoto mjini Paris

1573839
Mauaji ya genge la watoto nchini Ufaransa

Watoto 9 wenye umri wa kati ya miaka 13 na 18 wamewekwa kizuizini kwa kesi ya kumpiga na kumuua mtoto wa miaka 15 katika mji mkuu wa Paris nchini Ufaransa.

Magenge ya watoto yamekuwa yakiongezeka kila siku katika mji mkuu wa Paris nchin Ufaransa.

Wakitoa taarifa juu ya suala hilo ambalo linawatia wasiwasi viongozi wa Ufaransa, maafisa wa polisi walisema kwamba ushirika wa magenge unazidi kuongezeka miongoni mwa vijana wadogo.

Maafisa walielezea kuwa kuna ugumu wa kufuatilia magenge hayo kutokana na mawasiliano yao katika vikundi vilivyofungwa kupitia pogramu za simu za Snapchat au WhatsApp.

Inaaminika kwamba kuna takriban magenge 40 tofauti mjini Paris, haswa katika viunga vya kaskazini na mashariki.

Mapigano ya visu kati ya magenge yanatambulika kuwa mengi zaidi kuliko kipindi cha zamani.Habari Zinazohusiana