Akaunti ya YouTube ya Trump yasitishwa

Google yasitisha akaunti ya YouTube ya Rais wa Marekani Donald Trump

1562990
Akaunti ya YouTube ya Trump yasitishwa

Baada ya Facebook na Twitter, mtandao wa Google umesitisha akaunti ya YouTube ya Rais wa Marekani Donald Trump kwa sababu ya vurugu zilizotokea katika jengo la Bunge.

Trump alikuwa na wafuasi milioni 2.77 kwenye akaunti yake ya YouTube.

Kufuatia hatua iliyochukuliwa na kampuni hiyo, Trump hataweza kuchapisha video kwenye tovuti kwa muda usiopungua siku 7.

Mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook pia ilisitisha akaunti ya Trump.Habari Zinazohusiana