Mashambulizi ya silaha nchini Marekani
Watu 7 washambuliwa kwa silaha na kufyatuliwa risasi katika mji wa Chicago

Watu 5 kati ya 7 waliofyatuliwa risasi na mshambuliaji mmoja katika mji wa Chicago nchini Marekani wameripotiwa kupoteza maisha.
Polisi wa Chicago wallitoa maelezo na kufahamisha kwamba wahanga 7 walishambuliwa na kufyatuliwa risasi na mshambuliaji aliyetambulika kwa jina la Jason Nightengale nyakati tofauti za siku, ambapo watu 5 kati yao wamefariki.
Miongoni mwa wahanga hao waliofariki, ni mwanafunzi wa chuo kikuu, mfanyakazi wa mgahawa na walinda usalama ambao wawili ni wanawake.
Ilisemekana kwamba Jason Nightengale, ambaye alikabiliwa na polisi, alikuwa tayari na rekodi za mashtaka ya uhalifu.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32 amekamatwa na kushtakiwa mnamo 2005, kwa kesi za "ukiukaji wa sheria, mauaji ya bunduki,ulanguzi wa madawa ya kulevya, wizi na tabia za unyanyasaji wa nyumbani."
Habari Zinazohusiana

Ajali ya treni ya abiria Pakistan
Mmoja afariki, 40 wajeruhiwa kwenye ajali ya treni ya abiria iliyotokea nchini Pakistan