UN yampongeza Rais Tatar

Katibu Mkuu wa UN atuma ujumbe wa pongezi kwa Rais wa KKTC Ersin Tatar

1519121
UN yampongeza Rais Tatar

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres, amempongeza Ersin Tatar kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Kituruki ya Cyprus ya Kaskazini (KKTC).

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na ofisi ya rais, iliarifiwa kuwa Guterres alimtumia Tatar ujumbe wa pongezi na kusherehekea ushindi wake wa kuteuliwa kama kiongozi wa jamii ya Kituruki ya Cyprus.

Katika ujumbe huo, Guterres pia aliashiria mpango wa kujumuika pamoja kwa Tatar na kiongozi wa utawala wa jamii ya Cyprus ya Ugiriki Nikos Anastasiadis kwenye mkutano utakaofanyika tarehe 3 Novemba jioni kwa matumaini ya kuweka ushirikiano.

Katibu Mkuu Guterres pia alielezea matarajio yake ya kuwashirikisha  rais Tatar, Anastasiadis pamoja na mataifa husika kwenye mkutano wa wanachama 5 wa UN utakaofanyika.

Tatar alichaguliwa kuwa rais wa awamu ya 5 wa KKTC baada ya kushinda asilimia 51.69 ya kura kwenye duru ya pili ya uchaguzi iliyofanyika tarehe 18 Oktoba na kuanza kuhudumu rasmi tarehe 23 Oktoba.  Habari Zinazohusiana