Zoezi la wanajeshi wa Qatar lakamilika

Vikosi vya Wanajeshi vya Qatar, vilifanya mazoezi ya kijeshi kwa ushrikiano wa jeshi la Uturuki "NASR 2020" na mazoezi hayo sasa yamemalizika

1518421
Zoezi la wanajeshi wa Qatar lakamilika

Vikosi vya Wanajeshi vya Qatar, vilifanya mazoezi ya kijeshi kwa ushrikiano wa jeshi la Uturuki "NASR 2020" na mazoezi hayo sasa yamemalizika.

Kulingana na taarifa iliyoandikwa kutoka kwa Wizara ya Ulinzi ya Qatar, zoezi hilo lilikamlika kwa sherehe iliyohudhuriwa na Mkuu wa Jesh la Qatar Luteni Jenerali Ganim bin Shahin al-Ganim, Balozi wa Uturuki Doha, Balozi Mehmet Mustafa Goksu na makamanda wengine wakuu.

Mkurugenzi wa zoezi hilo, Meja Jenerali Hamed bin Ahmed en-Naimi, katika hotuba yake kwenye hafla hiyo, alisema kuwa zoezi hilo lilifanywa na ushiriki wa vitengo vyote vya vikosi vya jeshi na kikundi cha vikosi vya jeshi vinavyojiunga na Vikosi vya Wanajeshi vya Uturuki.

Akielezea kuwa zoezi hilo lilianza mnamo Juni 30 na kupita katika hatua kadhaa, Naîmi alisema kuwa Vikosi vya Jeshi la Qatar vina uwezo wa kupanga na kutekeleza operesheni za pamoja kwa nguvu na kwa uwezo mkubwa.Habari Zinazohusiana