Bolivia yafutilia mbali agizo la kumkamata Rais wa zamani

Agizo la kumkamata Rais wa zamani wa Bolivia lafutiliwa mbali na mahakama

1516951
Bolivia yafutilia mbali agizo la kumkamata Rais wa zamani

Bolivia imetangaza kufutilia mbali agizo la kumkamata Rais wa zamani wa nchi Evo Morales lililotolewa Desemba 2019.

Jaji mkuu wa mahakama ya sheria ya mkoa wa La Paz Jorge Quino, alitoa maelezo kwenye kituo cha televisheni cha Unitel, na kutangaza kufutiliwa mbali kwa agizo la kumkamata Morales aliyekuwa akiandamwa na kashfa ya ghasia na ufadhili wa magaidi.

Quino alielezea kuwa baadhi ya madai hayo yalikuwa na makosa baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina, na kuonekana kumnyima Morales haki ya kujitetea kisheria.

Wakati huo huo, agizo la kumkamata Waziri wa zamani wa sheria Hector Arce kwa madai ya ulaghai kwenye uchaguzi wa tarehe 20 Oktoba 2019 pia lilifutiliwa mbali.

Hector Arce, mawaziri kadhaa pamoja na baadhi ya viongozi serikali wamekuwa katika ubalozi wa Bolivia nchini Mexico kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa.Habari Zinazohusiana