Mgogoro wa makundi ya raia Marekani

Wafuasi wa Trump na kundi linalompinga wazozana barabarani Marekani

1516207
Mgogoro wa makundi ya raia Marekani

Wakati zimesalia siku chache kabla ya uchaguzi wa urais wa tarehe 3 Novemba kufanyika nchini Marekani, mgogoro umeibuka mjini New York kati ya wafuasi wa Donald Trump, na kundi linalompinga rais huyo.

Makundi hayo mawili yalianza mgogoro mbele ya jengo la Trump Tower lililoko mtaa wa 5th Avenue ambapo wafuasi wa kundi moja la kuunga mkono watu weusi la ‘‘Black Lives Matter’’walikuwa wakitembea barabarani kwa pamoja.

Wafuasi wa Trump walifungua bendera kubwa ya Trump kuonyesha kumuunga mkono, na baadaye wakaanza kutuleana matusi yaliyoambatana na vita.

Maafisa wa polisi waliingilia kati mgogoro huo na kukamata wafuasi kadhaa kutoka makundi yote mawili yaliyohusika.

Makundi ya kumpinga Trump yamekuwa yakiandamana mara kwa mara tangu kutokea kwa mauaji ya raia mwenye asili ya Kiafrika George Floyd, kutokea mwezi Mei kwa kusababishwa na maafisa wa polisi nchini humo.Habari Zinazohusiana