Mzozo wa soko la hisa Iran

Wananchi wa Iran waandamana kupinga kushuka kwa thamani ya soko la hisa

1516173
Mzozo wa soko la hisa Iran

Watu wengi walikusanyika mbele ya bunge la Iran kwa maandamano ya kupinga kushuka kwa thamani ya ubadilishanaji kwenye soko la hisa nchini humo.

Waandamanaji hao waliokusanyika mbele ya jengo la bunge la Iran, walibeba mabango yaliyoandikwa msemo wa kiongozi wa kidini nchini humo Ali Khamanei, unaosema, ‘‘Mahali pazuri pa kuwekeza ni katika soko la fedha.’’

Inaarifiwa kuwa mwenyekiti wa soko la hisa Hasan Kalibaf Asil alikuwepo ndani ya jengo la bunge wakati waandamanaji hao wakiandamana.

Kutokana na kushuka kwa thamani ya ubadilishanaji, Rais wa nchi Hassan Rouhani, alitoa maelezo siku 3 zilizopita kama yale aliyowahi kutoa tarehe 6 Agosti,  na kushawishi wananchi kuwekeza katika soko la hisa.

 Rouhani alisema,

‘‘Kulingana na viashiria vya soko, hali ya soko la hisa itakuwa nzuri zaidi siku zijazo. Wananchi wanapaswa kuwekeza mali zao kwenye soko la hisa.’’

Tangu tarehe 9 Agosti hadi kufikia sasa, soko la hisa la Iran limebainishwa kushuka kwa kiwango cha asilimia 36.Habari Zinazohusiana