Shirika la WHO laomba msaada wa mabilioni kwa ajili ya chanjo

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) laomba karibu dola bilioni nyingine kusaidia chanjo ya kimataifa

1500550
Shirika la WHO laomba msaada wa mabilioni kwa ajili ya chanjo

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) laomba msaada wa karibu dola bilioni nyingine kusaidia chanjo ya kimataifa na mpango wa matibabu dhidi ya Covid-19.

Serikali, mashirika ya kimataifa na sekta binafsi zimeahidi karibu dola bilioni 1 katika mkutano huo kusaidia mpango wa chanjo na matibabu duniani.

ACT Accelerator inakusudia kutoa dozi bilioni 2 za chanjo, matibabu milioni 245 na vipimo milioni 500 ifikapo mwisho wa 2021 na hii itahitaji dola bilioni 35. Mpaka sasa zilikuwa zimepatikana dola bilioni 3.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres ametaka msaada wa dharura wa dola bilioni 15 ili kuendelea na kazi ya sasa ya mpango wa chanjo duniani.Habari Zinazohusiana