Viongozi wa EU kukutana leo mjini Brussels

Viongozi wa Baraza la Umoja wa Ulaya (EU) wanatarajia kukutana leo mjini Brussels nchini Ubelgiji

1500697
Viongozi wa EU kukutana leo mjini Brussels

Viongozi wa Baraza la Umoja wa Ulaya (EU) wanatarajia kukutana leo mjini Brussels nchini Ubelgiji ambapo watajadili masuala mengi ukiwemo uhusiano kati ya Uturuki na EU, hali inayojiri Mediterania Mashariki na uongozi wa Belarus.

Mahusiano ya kigeni ni mada zitakazojadiliwa kwa sana katika mkutano wa Baraza la EU leo na kesho.

Mbali na mada ya Uturuki, Mediterania na Belarus, viongozi hao pia watagusia mapigano yanayoendelea kati ya Azerbaijan na Armenia huko Nagorno-Karabakh na vilevile mpinzani wa Urusi aliyepewa sumu Navalnıy Aleksey.

Mada kuhusiana na uchumi baada ya Covid-19, kuimarisha soko moja, kukuza sera bora zaidi za viwanda na mabadiliko ya kidijitali nazo zipo kwenye ajenda ya mkutano huo.

 Habari Zinazohusiana