Mtoto auawa katika mapigano Kashmir

Msichana amepoteza maisha kwenye shambulizi la risasi la wanajeshi wa India katika sehemu ya Kashmir inayodhibitiwa na Pakistani.

1490455
Mtoto auawa katika mapigano Kashmir

Msichana amepoteza maisha kwenye shambulizi la risasi la wanajeshi wa India katika eneo la Kashmir linalodhibitiwa na Pakistani.

Jeshi la Pakistani limeripoti kwamba wanajeshi wa India walifyatua risasi "bila sababu" kwenye vijiji vya mpaka wa Pakistani Hotspring na Rakhchikri Ijumaa usiku.

Imeelezwa kuwa msichana wa miaka 11 amepoteza maisha, na wanakijiji 4, akiwemo mwanamke wa miaka 75, wamejeruhiwa vibaya.

Kwa mujibu wa habari, jeshi la Pakistani lilijibu shambulizi hilo la wanajeshi wa India.

Wizara ya Mambo ya nje ya Pakistan pia imetangaza kuwa mwakilishi wa kidiplomasia wa India ameitwa wizarani kutokana na shambulizi hilo.

Msemaji wa jeshi la India Luteni Kanali Devender Anand amebainisha kuwa jeshi la Pakistani lililenga sehemu kadhaa za jeshi la India mpakani siku ya Jumamosi na Jumapili, na kwamba askari wa India "wamelipiza kisasi" dhidi ya shambulizi hilo , na kuongeza kuwa hakukuwa na majeruhi au vifo kwa upande wa India.Habari Zinazohusiana