Nepal yaandamwa na maporomoko ya ardhi

Watu 12 wamepoteza maisha katika maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa, nchini Nepal

1490421
Nepal yaandamwa na maporomoko ya ardhi

Watu 12 wamepoteza maisha katika maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa, nchini Nepal

Watu wasiopungua 21 hawajulikani walipo.

Maafa hayo yamekumba vijiji vitatu mashariki mwa mji mkuu, Kathmandu.

Wakati juhudi za uokoaji zikiendelea, kuna wasiwasi kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka.

Idadi ya watu waliopoteza maisha katika mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua za masika zilizoanza mnamo Juni huko Nepal imefikia watu 314.

Utawala wa Nepal umetangaza kuwa watu wasiopungua 111 bado hawajapatikana na watu 160 wameokolewa wakiwa na majeraha.Habari Zinazohusiana