Polisi waendelea kushambuliwa na Taliban

Polisi watatu wameuawa katika shambulizi la bomu lililofanywa na wanamgambo wa Taliban

1482773
Polisi waendelea kushambuliwa na Taliban

Polisi watatu wameuawa katika shambulizi la bomu lililofanywa na wanamgambo wa Taliban katika kituo cha polisi katikati mwa mkoa wa Paktiya nchini Afghanistan.

Msemaji wa Utawala wa Paktiya Abdulrahman Mangel amesema kuwa baada ya gari lililokuwa limebeba bomu kulipulika mlangoni mwa jengo hilo, wanamgambo wawili waliingia katika kituo cha polisi na kufyatua risasi ovyo.

Walinda usalama watano wameripotiwa kujeruhiwa.

Hata hivyo washambuliaji waliangamizwa ndani ya muda mfupi.

 Habari Zinazohusiana