Vifo vyaongezeka Pakistan

Mvua zimeendelea kunyesha kwa mfululizo nchini Pakistan toka tarehe 23 mwezi Agosti

1481309
Vifo vyaongezeka Pakistan

Mvua zimeendelea kunyesha kwa mfululizo nchini Pakistan toka tarehe 23 mwezi Agosti.

Idadi ya vifo kutokana na ajali zinazosababishwa na mafuriko inazidi kuongezeka siku hadi siku.

Mpaka hivi sasa, ni watu 63 wamepoteza maisha katika mvua hizo za masika.

Watu 47 wamepoteza maisha katika mafuriko hayo mjini Karachi.

Kumekuwa vilevile na usumbufu katika huduma za mawasiliano.

Inasemekana kuwa watumiaji wengi katika maeneo anuwai ya jiji hawawezi kupiga simu au kutuma ujumbe.

Usafiri wa umma pamoja na gari la wagonjwa vimeathiriwa vibaya na hali inayoendelea nchini humo.

Baadhi ya raia wameshindwa kurudi makwao na kulazimika kulala makazini au maeneo ya wazi , katika jiji la Karachi lenye watu milioni 15.

Timur Ali, Msemaji wa Wakala wa Usimamizi wa Maafa wa eneo la Khaybar Pahtunhva, amesema watu 16 wamefariki kutokana janga hilo katika jimbo lote.

Ali amesema kuwa nyumba 67 zimeharibiwa kutokana na maporomoko ya ardhi.Habari Zinazohusiana