Mgahawa waporomoka na kusababisha vifo China

Mgahawa wa ghorofa mbili umeporomoka na kusababisha vifo vya watu 13 Shanxi nchini China.

1481317
Mgahawa waporomoka na kusababisha vifo China

Mgahawa wa ghorofa mbili umeporomoka na kusababisha vifo vya watu 13 Shanxi nchini China.

Kulingana na kituo cha televisheni cha taifa nchini humo CCTV, tukio hilo limetokea katika mji wa Shiangfen, kilometa 630 kusini magharibi mwa mji mkuu Beijing.

Watu 30 wameokolewa baada ya kuwa wamefunikwa na kifusi huku wanne kati yao wakiwa wamejeruhiwa vibaya.

Mamia ya maafisa wanaendelea na shughuli za utafutaji na uokoaji.

Hakuna taarifa kamili kuhusu sababu kuu ya kuanguka kwa jengo hilo.

 Habari Zinazohusiana