Vifo kutokana na mafuriko vyaongezeka Pakistan

Idadi ya watu waliopoteza maisha katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika zilizonyesha mfululizo ndani ya siku tatu zilizopita

1480658
Vifo kutokana na mafuriko vyaongezeka Pakistan

Idadi ya watu waliopoteza maisha katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika zilizonyesha mfululizo ndani ya siku tatu zilizopita, imeongezeka na kufikia watu 34 Karachi nchini Pakistan.

Kulingana na kituo cha televisheni cha "Dunya News" nchini Pakistan, maeneo mengi yamefunikwa na maji na barabara kufurika.

Watu 23 zaidi wamepoteza maisha, hali iliyopelekea idadi ya vifo kuongezeka.

Timu za uokoaji zinaendelea na shughuli za kuwatafuta na kuwasaidia wale walioathirika kwa kiasi kikubwa na mafuriko hayo.

 

 Habari Zinazohusiana