Mashambulizi ya bomu Afghanistan

Raia kumi na tatu wameuawa katika mashambulizi mawili mfululizo ya bomu katika mkoa wa Kandahar kusini mwa Afghanistan.

1480994
Mashambulizi ya bomu Afghanistan

Raia kumi na tatu wameuawa katika mashambulizi mawili mfululizo ya bomu katika mkoa wa Kandahar kusini mwa Afghanistan.

Msemaji wa Gavana wa Kandahar, Bahir Ahmadi, amewaambia wanahabari kuwa mabomu mawili ya barabarani wilayani Kinehar yamelipuka mfululizo wakati gari mbili zilizokuwa zimebeba raia zilipopita katika eneo hilo.

Imeripotiwa kuwa watatu kati ya waliopoteza maisha ni watoto huku watu wengine watatu wakiwa wamejeruhiwa.

Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na mashambulizi hayo mpaka hivi sasa.

Kwa upande mwingine raia wawili wameuawa katika shambulizi la bomu katika mkoa wa Nangarhar.

Msemaji wa Gavana wa Nangarhar Ataullah Hogyani amesema kuwa bomu kando ya barabara ililipuka wakati baba na mwanawe walipokuwa wakipita katika kijiji cha Veziru wilayani Hogyani.

Baba na mtoto wamepoteza maisha katika mlipuko huo.Habari Zinazohusiana