Mafuriko yapelekea vifo vya watu 70 Afghanistan

Watu 70 wameripotiwa kupoteza maisha katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini Afghanistan.

1479716
Mafuriko yapelekea vifo vya watu 70 Afghanistan

Watu 70 wameripotiwa kupoteza maisha katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini Afghanistan.

Kwa mujibu wa habari, mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa katika mkoa wa Pervan karibu na Kabul, mji mkuu wa Afghanistan.

Kulingana na msemaji wa utawala wa Pervan, mafuriko hayo yamesababishwa na mvua iliyonyesha mfululizo kwa zaidi ya masaa ishirini na nne.

Watu wengine 100 wamesemekana kujeruhiwa.

Shughuli za uokoaji zinaendelea.Habari Zinazohusiana