Watu watatu wauawa katika shambulizi Afghanistan

Watu 3 wameuawa na 41 wamejeruhiwa katika shambulizi la bomu

1479061
Watu watatu wauawa katika shambulizi Afghanistan

Watu 3 wameuawa na 41 wamejeruhiwa katika shambulizi lililosababishwa na gari lililokuwa limetegwa bomu katika mkoa wa Balkh kaskazini mwa Afghanistan.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi, imeripotiwa kuwa mshambuliaji huyo alilenga kituo cha wilaya ya Belh kwa kutumia gari ilitegwa bomu.

Imeelezwa kuwa kati ya watu 3 waliopoteza maisha wawili walikua ni raia wa kawaidahuku watu wengine 41 wakiwa wameripotiwakujeruhiwa.

Majengo ya karibu ya mlipuko huo yameharibika kwa kiasi kikubwa.

Kuna hofu ya kuongezeka kwa idadi ya waliopoteza maisha.

Taliban imetangaza kuhusika na shambulizi hilo.

 Habari Zinazohusiana