Huenda watoto wachanga huuawa na madaktari

Matokeo ya utafiti yawaacha watu midomo wazi

1477229
Huenda watoto wachanga huuawa na madaktari

Matokeo ya utafiti uliofanywa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha George Mason juu ya viwango vya kupona vya watoto wachanga hospitalini nchini Marekani yamewashangaza wengi.

Utafiti huo, uliochapishwa katika Taasisi ya Kitaifa ya Sayansi ya Marekani,ulichambua data juu ya uzazi milioni 1.8 katika hospitali huko Florida kati ya mwaka wa 1992 na 2015.

Utafiti umegundua kuwa zoezi la kuzalisha watoto wachanga wa Kiafrika likifanywa na madaktari weupe, uwezekano wa kufa  kwa watoto hao unakua mara 3  ukilinganisha na watoto weupe.

Pale ambapo madaktari weusi huzalisha basi kiwango cha kufa kwa watoto wachanga wa Kiafrika hospitalini hupungua kati ya asilimia 39 na asilimia 58.

Watoto wa asili ya Kiafrika tayari wanajulikana kufa wakiwa wachanga mara 2.3 zaidi  kuliko watoto weupe.

Hii ni kulingana na Ofisi ya Afya ya Idara ya Watu wa Marekani.

Ripoti kutoka kwa Vituo vya Marekani vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, ilivyochapishwa mnamo Juni, na kuorodhesha kipindi cha 2000 hadi 2017, imegundua kuwa watoto wachanga wa Kiafrika bado walikuwa na uwezekano wa kufa mara mbili kuliko watoto weupe.Habari Zinazohusiana