Joto lapelekea vifo vya watu 79 Tokyo

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na hali ya hewa ya joto imeongezeka mpaka watu 79 huko Tokyo, mji mkuu wa Japan.

1475725
Joto lapelekea vifo vya watu 79 Tokyo

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na hali ya hewa ya joto imeongezeka mpaka watu 79 huko Tokyo, mji mkuu wa Japan.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya kitaifa, Ofisi ya Tokyo ya Ustawi wa Jamii na Afya ya Umma imetoa data mpya juu ya wale waliopoteza maisha kutokana na joto kali.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, jumla ya watu 79 wamepoteza maisha 70 kati yao wakiwa na umri wa zaidi  ya miaka 65.

Watu hao wamepoteza maisha tangu mwanzoni mwa mwezi Agosti.

Joto katika mji mkuu wa Japani limetanda kati ya nyuzi 32 hadi 37 tangu mwisho mwa mwezi Julai.


Tagi: #Tokyo , #joto , #vifo

Habari Zinazohusiana