Mamia wapoteza maisha katika mafuriko India

Angalau watu 868 wamepoteza maisha katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa mwaka huu nchini India.

1474528
Mamia wapoteza maisha katika mafuriko India

Angalau watu 868 wamepoteza maisha katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa mwaka huu nchini India.

Kulingana na ripoti ya Hindustan Times, ripoti ya kitengo cha Wizara ya Mambo ya Ndani cha kukabiliana na majanga  ya tarehe 12 Agosti, imebainika kuwa watu 868 wamepoteza maisha katika majimbo 11 hadi sasa kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na msimu wa monsoon wa mwaka wa 2020.

Ripoti imeendelea kusema kwamba idadi hii ilikuwa 908 katika kipindi kama hicho cha mwaka jana.

RK Jenamani wa Kituo cha Utabiri wa hali ya hewa cha Taifa amesema kwamba mwaka huu wameshuhudia mvua za ajabu na matukio kadhaa ya hali ya hewa kali,

"Kwa mfano, mji katika mkoa wa Jaipur ulinyesha milimita 250 za mvua katika masaa 6."

Wakati huo huo, mamia ya maelfu ya watu ambao waliachwa bila makazi kutokana na mafuriko yaliyoharibu maelfu ya hekta za ardhi ya kilimo, nyumba na barabara wamepatiwa makazi.

Mvua za kati ya  Juni-Septemba mara nyingi  husababisha majanga makubwa ya asili na ajali kila mwaka katika Kusini mwa Asia.Habari Zinazohusiana