Maafisa Usalama washambuliwa Afghanistan

Maafisa usalama 7 wamepoteza maisha katika shambulizi kwenye kitengo cha jeshi katika mkoa wa Ghazni nchini Afghanistan.

1469613
Maafisa Usalama washambuliwa Afghanistan

Maafisa usalama 7 wamepoteza maisha katika shambulizi kwenye kitengo cha jeshi katika mkoa wa Ghazni nchini Afghanistan.

Kitengo hicho cha jeshi kinasemekana kuwa kimeshambuliwa na gari iliyokua imetegwa bomu.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Tarık Aryen amesema kuwa kitengo cha jeshi katika mkoa wa Kotal Ravza huko Gazne kimeangamizwa na gari iliyotegwa bomu.

Aryen amesema kuwa walinzi wa usalama 7 wamepoteza maisha na walinzi 16 wamejeruhiwa katika shambulizi hilo.

Bado hakuna mtu ambaye amedai kuhusika na shambulizi hilo.Habari Zinazohusiana