Coronavirus: Zaidi ya watu   milioni 18,7  wameambukiwa ulimwenguni

Idadi ya watu ambao wamekwishamabukiwa virusi vya corona ulimwenguni imefikia watu  zaidi ya milioni 18,7

1468035
Coronavirus: Zaidi ya watu   milioni 18,7  wameambukiwa ulimwenguni


Idadi ya watu ambao wamekwishamabukiwa virusi vya corona ulimwenguni imefikia watu  zaidi ya milioni 18,7.

Idadi ya watu ambao wamekwishaambukiwa virusi vya corona ulimwenguni, idadi yake imefikia watu  milioni  18,7 huku  idadi ya watu waliofariki ikiripotiwa kufikia watu   704 632.

Idadi ya jumla ya watu ambao wamekwishapona vilevile baada ya kupatiwa matibabu  inaendelea kuongezeka, idadi hiyo imefahamishwa kufikia watu   zaidi ya   milioni 11,9 kote ulimwenguni.

Nchini Marekani, watu   zaidi ya 160 318 wamekwishafariki tangu kuanza kwa janga hilo mwishoni mwa mwaka 2019 huku idadi ya watu walioambukiwa virusi hivyo idadi yake imefikia watu milioni 4,9.

Rais Trump  amezungumza kuhusu idadi  hiyo ya watu wanaoendelea kufariki  na kusema kwamba haina maana kuwa serikali haitekelezi wajibu wake , serikali inafanya kila liwezekanalo kukabiliana na janga hilo.

Mshauri wa White House, Robert O Biren ambae aligunduliwa kuwa na maambukizi  amepimwa kwa  mara nyingine na kukutwa ypo salama  na sasa tayari amerejea ofisini kwake kutekeleza wajibu wake.

Nchini Brazil,  watu  96 096 wamefariki kwa covid-19,  watu  1154 wamefariki  ndani ya siku moja.

Nchini Mexico, watu  48 869 wamefariki, idadi hiyo imeonegezeka baada ya watu  857 kufariki ndani ya masaa 24 yaliopita.

Nchini Uingereza, watu  46 299 wamefariki kwa covid-19.

Nchini Ugiriki , watu  209 wamefariki, watu  4855 wamegunduliwa kuwa na maambukizi ndani ya masaa 24.

Nchini Italia, watu 35 171 wamekwishafariki, nchini Canada watu  8959 huku Australia ikiwa nawatu  247 waliofariki tangu kuanza kwa janga hilo.Habari Zinazohusiana