Vifo vyaongezeka Lebanon

Vifo kutokana na milipuko vyafikia 113

1467751
Vifo vyaongezeka Lebanon

Idadi ya watu waliofariki katika milipuko iliotokea mjini Beyruth nchini Lebanon yazidi kuongezeka.

Mjini Beyruth nchini Lebanon milipuko miwili mikubwa ilitokea Jumanne majira ya jioni imepelekea vifo vya watu kufikia 113 na wengine zaidi ya  4000 kujeruhiwa.

Milipuko hiyo imeripotiwa kutokea katika hifadhi ya bidhaa tofauti  katika bandari ya mjini humo Beyruth.

Kulingana na taarifa zilizotolewa ni kwamba milipuko hiyo imesababishwa na  madini ya "Nitrate ya Amonium" madini ambayo yanauwezo wa kulipuko  kama yatakuwa hayakuhifadhiwa vizuri.

Zaidi ya ghala 12 zimeteketea na moto katika milipuko hiyo  iliosababisha hasara kubwa nchini Lebabon.

Mjumba  mengi yameharibiwa licha ya kuwa mbali na eneo la tukio  bandari ya Beyruth.

Hospitali mjini humo  zimekumbwa na uhaba wa nafasai za kuwapokea majeruhi na madawa.

Taarifa za awali zimefahamisha kwamba miongoni mwa watu waliojeruhiwa wamo raia wawili wa Uturuki.

Nyumba  ya waziri mkuu wa Lebanon Saad Hariri na majumba mengine ya serikali  yameathirika katika milipuko hiyo.Habari Zinazohusiana