Safari za ndege kutoka Urusi kuelekea Uturuki zaanza upya

Safari za ndege kutoka nchini Urusi kelekea nchini Uturuki baada ya kusitishwa kutokana  na covid-19 zaanza upya

1465533
Safari za ndege kutoka Urusi kuelekea Uturuki zaanza upya


Safari za ndege kutoka nchini Urusi kelekea nchini Uturuki baada ya kusitishwa kutokana  na covid-19 zaanza upya.

Kutokana  na mlipuko wa janga la virusi vya corona,  mipaka kati ya mataifa tofauti ulimwenguni  ilifungwa katika jitihada za kuzuia maambuzi ya virusi vya corona mwanzoni mwa mwaka  2020.

Uturuki ni miongoni mwa mataifa mabyo yalifunga mipaka yake kwa lengo la kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Safari za ndege kutoka katika uwanja wa  ndege wa Vnukovo  nchini Urusi  zimeanza  kuelekea nchini Uturuki.

Ndege ya shirika  la ndege la Uturuki la THY Turkish Airlines imeondoka  katika uwanja huo wa ndege ikiwa na abiria kutoka  Urusi kuelekea Uturuki.

Watu  hoa waliosafiri kuelekea Uturuki wamefahamisha kwamba wanajielekea  mjini Antalya kupitia mjini Istanbul kwa ajili  ya likizo katik a msimu wa  kiangazi.

Usalama umeimarishwa  katika uwanja wa ndege huku abiria wote wameomba kuheshimu uvaaji wa barakoa na kuzingatia usafi.Habari Zinazohusiana