Oktay : "Kamwe hatutowasahau waliendesha mauaji ya kimbari Srebrenitsa"

Makamu wa rais wa Uturuki asema kwamba kamwe Uturuki haitowasahau walioendesha mauaji ya kimbari ya Srebrenitsa

1453424
Oktay : "Kamwe hatutowasahau waliendesha mauaji ya kimbari Srebrenitsa"


Makamu wa rais wa Uturuki asema kwamba kamwe Uturuki haitowasahau walioendesha mauaji ya kimbari ya Srebrenitsa.

Fuat Ooktay, makamu wa rais wa  Uturuki amesema kwamba kamwe Uturuki haitowasahau walioendesha mauaji ya kimbari ya Srebrenitsa mwakka  1995.

Watu wasiopungua 8 000 waliuawa katika mauaji hayo ya mwaka  1995 walioweka doa baya katika historia ya Ulaya.

Oktay amesema kuwa  waboznia zaidi ya 8 000 waliuawa katika  vita hivyo ambavyo vilianzishwa dhidi ya waboznia.

Vile vile makamu huyo wa rais wa Uturuki amesema kuwa  waliofumbia macho mauaji hayo pia kamwe hawatosahauhalika.

Nakamu wa rais wa Uturuki, Fuat Oktay ameandika katika  kurasa zake  katika mitandao ya kijamii katika maadhimisho ya miaka 25 tangua kufanyika kwa mauaji ya kimbari  ya Srebrenitsa mwaka  1995.

Oktay amekumbusha maneno  ya rais wa kwanza wa Boznia Herzegovina  huru Alija Izetbegovic ambae alisema kwamba " hatutosahau kamwe mauaji  ya kimabari ya Srebrenitsa laa sivyo  yatatokea kwa mara nyingine".Habari Zinazohusiana