Idadi ya visa vipya vya maambukizi ya covid-19 ulimwenguni

Watu zaidi ya 508250 wamekwishafariki   kutokana na virusi vya corona ulimwenguni

1445960
Idadi ya visa vipya vya maambukizi ya covid-19 ulimwenguni

Ni watu zaidi ya  508250  ulimwenguni ndio ambao wameripotiwa  kufariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona  tangu kuanza kwake katika jimbo la Wuhan nchin China mwishoni mwa mwaka 2019.

Watu milioni 10,4 wameripotiwa  kuwa na maambukiz ya virusi hivyo huku idadi ya watu ambao wamepona baada ya kupatiwa matibabu ikiripotiwa kuwa watu   milioni  5,6.

Nchini Marekani , watu  128 783 wamekwishafariki kutokana na  virusi hivyo  huku pia watu   milioni 2,6 na zaidi wakiwa wameshamabukiwa virusi hivyo vya  covid-19.

Nchini humo baadhi ya viongozi wa chama cha "Demokrat" wanamshikiza rais wa taifa hilo Donald Trump  kutoa amri chini ya misingi ya sheria   ya kulazimu kuvaa barakoa katika majimbo yote ya Marekani.

Hadi sasa ni majimbo  18  nchini humo ambayo yanawaimiza raia wake kuvaa barakoa.
 Nchini Brazil, watu  692 wamefariki  ndani ya masaa  24  na kupelekea idadi ya vifo kufikia watu   52314 huku visa vya maambukizi vikiripotiwa kufikia  watu   milioni 1,3 baada ya watu wengine kupimwa na kugunduliwa kuwa na maambukizi.
Nchini Mexico, watu 27112.Habari Zinazohusiana