Sudani yasitisha safari za ndege kutokana na maambukizi ya covid-19

Sudani yasitisha safari za ndege kutokana na maambukizi ya virusi vya corona

1444937
Sudani yasitisha safari za ndege kutokana na  maambukizi ya covid-19

Idadi ya watu ambao wamefakwishafariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona  ulimwenguni imefikia watu zaidi ya 501 000 tangu  kaunza kwake mwishoni mwa mwaka  2019 katika jimbo la wuhan nchini China.

Idadi pia ya watu ambao wamepona maambukizi ya virusi vya corona  pia imeripotiwa  kuongezeka  na kufikia watu  milioni 5,4.

Nchini India , watu  384 wamefariki na kupelekea idadi ya vifo kuongezekana na kufikia watu  16112.

Idadi  hiyo ya  watu  384 wamefariki ndani ya masaa  24. Idadi ya watu wwaliopona  katika Ukanda huo wa Asia na Mashariki ya Kati  pia inaongezeka.

India ni ndio taifa ambalo  linashika nafasi ya  4  kwa maambukizi ya virusi vya corona.

Nchinİ Iran tangu kuanza kwa janga hilo ni watu  10 508 wamefariki  na idadi ya watu  ambao wameambukiwa  virusi hivyo imefikai watu  222669.

Rais wa Iran Hasan Ruhani  amesema kwamba   katika kipindi cha  wiki mbili zijazo   uvaaji wa barakao utahimizwa  kwa raia wote .

Hadi kufikia sasa ni watu  9073  wamefariki   nchini Urusi  huku idadi ya watu walioambukiwa ikifahamishwa kufikia watu   634437.

Nchini Irak, watu  101 wamefariki ndani ya masaa  24 na idadi ya watu   waliofariki pia meripotiwa kuzidi kuongezeka.

Barani Afrika,   ni watu zaidi ya   374 596 ndio ambao wameambukiwa virusi hivyo.
Nchini Misri, watu  2708 wamefariki tangu kuanza kwa janga hilo,  miskiti iliokuwa imefungwa kwa muda wa miezi mitatu sasa imeanza kufunguliwa.

Miskiti hiyo  ilifungwa kutokana na  hatua zilizochukuliwa katika kupambana  na maambukizi ya virusi hivyo.

Nchini Sudani safari za ndege zimezuiliwa kutokana na maambukizi ya covid-19 hadi ifiikapo Julai 12 . Nchini humo ni watu  572 ndio ambao wamekwishafariki.

Idadi ya watu ambao wamefariki katika mataifa ya Mashariki ya Kati na Asia ya Kati ni kama ipasavyo :

Nchini China watu 4634, nchini Pakiastani  watu  4118, Indonesia 2720, Afrika Kusini watu  2413, Bangladesh watu  1695, Saudia watu  1511, Ukraina 1129 , Qatar watu  110 , Georgia watu  15 naa nchini Kazakistani watu  166.


Tagi: #Asia , #corona

Habari Zinazohusiana