Uturuki yatoa msaada wa vifaa vya matibabu nchini Paraguay

Uturuki metuma msaada wa vifaa vya matibabu na madawa nchini Paraguay

1442017
Uturuki yatoa msaada wa vifaa vya matibabu nchini Paraguay


Uturuki metuma msaada wa vifaa vya matibabu na madawa nchini Paraguay.

Uturuki imetuma vifaa vya matibabu na madawa nchini Paraguay katika kuonesha ushirikiano na mataifa mabyo yanahitaji msaada katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

Paraguay ni moja ya mataifa Afrika ya Kusini ambayo yameathirika na maambukizi ya virusi hivyo hatari.

Mke wa rais wa Paraguay Silvana Abdo ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa  msaada wa vifaa vya matibabu  umewasili nchini  kutoka nchini Uturuki.

Katika ujumbe wake huo  shukrani zimetolewa kwa  Uturuki na rais wake kwa msaada huo katika kipindi hiki kigumu cha kupamaba na maambukizi ya virusi vya corona.

Mke wa rais wa Paraguay amempongeza pia mke wa rais Erdoğan Bi Emine Erdoğan kwa kuonesha moyo wa ushirikiano.

Msaada huo  ni pamoja na  barakoa 30 000 aina ya N95, barakoa  100 000 na vifaa vingene muhimu kwa wauguzi katika  kukabiliana na maambukizi ya covid-19.Habari Zinazohusiana