Safari za ndege kutoka Uturuki kuelekea Iran kuanza

Waziri wa mambo  ya nje wa Uturuki  amepokea waziri wa mambo ya nje wa Iran na kuzungumza kuhusu safari za ndege kutoka Uturuki kuelekea nchini Iran

1436808
Safari za ndege kutoka Uturuki kuelekea Iran kuanza


Waziri wa mambo  ya nje wa Uturuki  amepokea waziri wa mambo ya nje wa Iran na kuzungumza kuhusu safari za ndege kutoka Uturuki kuelekea nchini Iran.

Waaziri wa mambo ya nje wa Iran Jawad Zarif amefanya ziara rasmi nchini Uturuki na kuzungumza na waziri w amambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu.

Katika mzungumzo yaliofanyika kati ya mawaziri hao wawili,  suala kuhusu safari za ndege  kati ya mataifa  hayo mawili  limejadiliwa.

Katika mkutano na waandishi wa habari baada ya  mazungumzo yao, waziri wa mambo ya nje wa Uturuki amesema kwamba safari za ndge kutoka  Uturuki kuelekea nchini Iran  zitaanza ifikapo Agosti Mosi.

Mkutano huo na waandishi wa habari ulifanyika baada ya kumaliza mazungumzo yao.

Ziara hiyo ya waziri wa mambo ya nje wa Iran nchini Uturuki ni ziara ya kwanza  tangu kuanza kwa janga la virusi vya corona mwanzoni mwa mwaka  2020 .

Iran ilichukuwa hatua  ya kusitisha safari zake  kutokana na covid-19 na  kwa lengo la kuzuia maambukizi.Habari Zinazohusiana