Rais Erdoğan awatakia Eid njema viongozi mbalimbali

Eid al-Fitr na viongozi tofauti ulimwenguni

1423344
Rais Erdoğan awatakia Eid njema viongozi mbalimbali

Rais Recep Tayyip Erdoğan amefanya mazungumzo na viongozi wa nchi kadhaa akiwatakia kheri ya sikukuu ya Eid al-Fitr.

Kulingana na taarifa kutoka ikulu ya rais mjini Ankara,Rais Erdoğan amefanya mazungumzo ya simu na Rais wa Irani Hasan Ruhani, Rais wa Pakistani Arif Alvi, Rais wa Turkmenistan Gurbangulu Berdimuhamedov, Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev na Sultan wa Oman Haitham bin Tarıq.

Wakati wa mazungumzo hayo Erdoğan amewapa wote salamu za Eid,na kujadili masuala mengine tofauti kama masuala ya kikanda,ushirikiano na mapambano dhidi ya virusi vya corona.

 Habari Zinazohusiana