Ajali ya ndege yaua watu 97 Pakistan

Karibu watu 97 wamepoteza maisha katika ajali ya ndege Karachi nchini Pakistan

1422256
Ajali ya ndege yaua watu 97 Pakistan

Karibu watu 97 wamepoteza maisha katika ajali ya ndege Karachi nchini Pakistan.

Watu wawili wamenusurika.

Ndege ya kimataifa ya Pakistan International Airlines (PIA) PK-8303, ikisafiri kutoka kaskazini mashariki mwa Lahore, ilianguka katika eneo la makazi karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jinnah wakati ilipokuwa ikitua ikiwa imebeba abiria 99 na wafanyakazi.

Ajali hiyo imetokea siku kadhaa baada ya kuruhusiwa tena kuanza tena kwa ndege za ndani ya nchi kufuatia kizuizi cha mwezi mzima kilichowekwa kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

Waziri Mkuu Imran Khan amramuru uchunguzi juu ya ajali hiyo ya ndege ambayo ni ya pili tangu 2016.

Idara ya afya imethibitisha kuwa watu 20 waliojeruhiwa wapo katika hali mbaya.

Mamlaka, haikuweza kutambua hapo awali kama watu waliopoteza maisha na kujeruhiwa walikuwa ni abiria au wakazi wa eneo ilipoanguka ndege hiyo.Lakini baadaye imewekwa wazi kuwa wale wote waliopoteza maisha walikuwa ni abiria wa ndege hiyo huku baadhi ya wakazi wakiwa wamejeruhiwa.

Wakazi wengi wa eneo la ajali wamehamishwa kutokana na nyumba zao kuharibiwa vibaya.

Miili 19 imeweza kutambuliwa huku mingine ikiwa katika hali isiyoweza kutambulika.

Abiria hao walikuwa wakisafiri kusherehekea sikukuu ya Eid-ul-Fitr ikiwa ni siku za mwisho za mwezi mtukufu wa Ramadhan.Habari Zinazohusiana