Virusi vya corona ulimwenguni

Idadi ya watu ambao wamekwishafariki kutokana na virusi vya corona katika pembe nne za dunia imeripotiwa kufikia watu   316 800

1419275
Virusi vya corona ulimwenguni

Idadi ya watu ambao wamekwishafariki kutokana na virusi vya corona katika pembe nne za dunia imeripotiwa kufikia watu   316 800 huku idadi ya   watu walioambukiwa ikiwa imefikia watu   zaidi ya miloni 4,8.

Taarifa zilizotolewa kutoka  katika mataifa tofauti, kwa  pamoja watu ambao wamekwishapona  imefikia watu   863 200.

Nchini Marekani watu  90970 wamefariki kutokana na virusi vya corona, 
Daktari  mmarekani mwenye  asili ya Moroko, Moncef Slaoui ambae ameanzisha  mpango ambao una matumaini ya kufikia kunako chanjo dhidi ya Corona amewavutia wengi.

Daktari huyo anajulikana kama   mtaalamu wa chanjo wa kimataifa.

Idadi ya watu ambao  wamefariki nchini Uingereza  imefikia watu  34636 baada ya watu  170 lkufariki ndani ya masaa  24.

Nchini Italia, watu   walioafriki kwa virusi vya corona  imefikaia watu  31908 baada ya watu  145 kufariki ndani ya masaa 24.

 Vyombo vya habari nchini humo vimetangaza kupona kwa mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 104  ambae alikuwa ameambukiwa covid-19.

Mwanamke huyo amapona baada ya kupatiwa matibabu.

Nchini Ufaransa, watu  483 wamefariki ndani ya masaa  24 na kupelekea idadi ya vifo  kufikia watu   28108 .

Vifo kutokana na virusi vya corona katika mataifa mengine ulimwenguni :

Uhispania ni watu  27 650, nchini Brazil watu   16122, Ubelgiji  9052,  Ujerumani watu   8049,  nchini Canada 5782, Uholanzi watu   5,680, Mexico 5177, Uswisi 3679, Peru  2648, Chile watu   450.Habari Zinazohusiana