Uturuki yawahamisha raia wake kutoka Tanzania

Wawekwa karantini siku 14

1418729
Uturuki yawahamisha raia wake kutoka Tanzania

Raia wa Uturuki wamehamishwa kutoka Ujerumani na Tanzania mapema Jumapili na kuwekwa chini ya kizuizi(karantin) cha siku 14 ili kupunguza kuenea kwa virusi vya corona.

Jumla ya Waturuki 157 kutoka Ujerumani wamepelekwa mkoa wa Kayseri na baadaye kupelekwa katika mabweni ya wanafunzi kwa ajili ya karantini baada ya ukaguzi wa kiafya.

Halikadhalika, Uturuki imewarudisha raia 53 kutoka Tanzania.

Walifika Ankara kwa safari ya ndege na walipelekwa Kirikkale kufuatia taratibu kama zilizowekwa mjini Kayseri.

Uturuki imerudisha karibu watu 70,000 kutoka mataifa 107, chini ya maagizo ya Rais Recep Tayyip Erdoğan na kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya nje.

Ankara iliripoti kesi 148,067 za virusi vya corona siku ya Jumamosi, huku watu 108,137 wakiwa wamepona kabisa. Idadi ya vifo imefikia 4,096.

Zaidi ya kesi milioni 4.63 zimeripotiwa katika nchi 188 tangu virusi hivyo kutokea nchini Uchina Desemba mwaka jana, na maeneo yalioathirika zaidi yakiwa Marekani na Ulaya.

Sehemu kubwa ya wagonjwa wa COVID-19, karibu milioni 2, wamepona, lakini virusi hivyo vimechukua  zaidi ya maisha 311,000, kulingana na data iliyokusanywa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins cha Marekani.Habari Zinazohusiana