Ronaldinho azungumza kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwake

Nyota wa zamani wa kabumbu wa Brazil Ronaldinho azungumza kwa mara ya kwanza tangu  kukamatwa  nchini  Paraguay

1406765
Ronaldinho azungumza kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwake


Nyota wa zamani wa kabumbu wa Brazil Ronaldinho azungumza kwa mara ya kwanza tangu  kukamatwa  nchini  Paraguay.

Ronaldinho , nyota wa kabumbu kutoka nchini Brazil na klabu kadhaa barani Ulaya alikamtwa mpakani mwa Paraguay akijaribu kuingia nchini humo akiwa na hati ya kusafiri isiokuwa yake.

Tulishtusha sana kuona tunakamatwa na kutupwa gerezani kwa kosa la kutumia hati za kusafiria  zisizokuwa milki yetu amesema Ronaldinho  kipindi  alipokuwa akihojiwa kuhusu tukio hilo baada ya kuzuiliwa.

Ronaldinho amesema kuwa alijaribu mara  kadhaa kufafanua  na kuweka wazi kuhusu  kitendo hicho, nilishtusha  kuona nahukumiwa adhabu ya kifungo gerezani ni jambo ambalosikuwahi kufikiria katika maisha yangu ameendelea  kufahamisha Ronaldinho.

Katika  mahojiano yake  hayo , Ronaldinho  hajamsahau mama yake kwa kusema kuwa  janga la virusi vya corona linamsumbua na kusema jambo la kwanza atakalofanya pindi atakapomalizi adhabu yake  atamkumbatia mama yake.

Ronaldinho na  ndugu yake Assis wamefungwa kifungo cha nyumbani baada ya kutoa kiwango cha dola milioni  moja na laki 6.Habari Zinazohusiana