Mkutano wa Umoja wa Ulaya kukabiliana na athari ya Covid-19 katika uchumi

Viongozi wa mataifa ya Umoja wa Ulaya wakutana  na kuzungumza kuhusu  kuzuia   kuathirika kwa sekta ya uchumi  kutokana na janga la virusi vya corona

1404596
Mkutano wa Umoja wa Ulaya kukabiliana na athari ya Covid-19 katika uchumi

Viongozi wa mataifa ya Umoja wa Ulaya wakutana  na kuzungumza kuhusu  kuzuia   kuathirika kwa sekta ya uchumi  kutokana na janga la virusi vya corona.

Viongozi hao wamekutana na kuzungumza mbinu zinazostahili katika juhudi za kuimarisha  uchumi na kuzuia kuporomoka katka kipindi hiki kigumu ambacha mataifa mengi tayari yamekwishaathirika  kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Mkutano huo umefanyika kwa njia ya video ukihudhuriwa na viongozi wa mataifa  27 wanachama wa Umoja huo.

Viongozi hao wanajaribu kujadiliana  ili kufikia katika maamuzi ya pamoja katika makabiliano dhidi ya Covid-19 ambayo inaathiri sekta ya uchumi katika mataifa wanacha wa Umoja wa Ulaya.

Imeripotiwa kuwa na hali ya kutoafikiana  katika mkutano huo  kutokana na athari ambazo zimekwishajitokeza  katika sekta ya  uchumi.

Italia, Uhispania na Ufaransa zimefahamisha kuomba mkakati wa pamoja  ili kukabiliana na  kuyumba kwa uchumi katika mataifa ya Umoja huo.

Mataifa kama Ujerumani, Uholanzi , Finlandia na Austria  yamepinga vikali mpango wa  deni la majumuu.Habari Zinazohusiana