Urusi kukubali kupunguza uzalishaji wa mafuta

Urusi itakubali kupunguza uzalishaji wa mafuta kwa mapipa milioni 1.6.

1394235
Urusi kukubali kupunguza uzalishaji wa mafuta

Urusi imetangaza kuwa itakubali kupunguza uzalishaji wa mafuta kwa mapipa milioni 1.6.

Kulingana na shirika la habari la TASS la Urusi, afisa kutoka Wizara ya Nishati amesema kuwa utawala wa Moscow utakubali kupunguza uzalishaji wa mafuta kwa mapipa milioni 1.6, chini ya makubaliano kati ya OPEC na nchi nyingine za wazalishaji zisizo za OPEC.

Afisa huyo amesema kuwa kupunguzwa kwa uzalishaji huo kutaambatana na asilimia 14 ikilinganishwa na robo ya kwanza ya 2020.

Saudi Arabia iliitisha mkutano wa dharura ili kuhakikisha "mpango mzuri" kati ya OPEC na nchi zisizoongozwa na OPEC.

Kwa hivyo imeamuliwa kufanyika mkutano kati ya OPEC na nchi zisizo za OPEC kupitia video tarehe mnamo 9 Aprili.Habari Zinazohusiana