Marufuku mpya ya "Whatsapp"

Whatsapp yapunguza kasi ya kutumiana ujumbe

1393271
Marufuku mpya ya "Whatsapp"

Toka mlipuko wa ugonjwa hatari wa Corona,kumekuwa na usambazaji wa haraka wa ujumbe kuhusu kirusi hiki katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Moja wapo ikiwa ni "Whatsapp".

Watu wameonekana wakitumia Whatsapp kutuma ujumbe wa haraka kwa jamaa na marafiki.Lakini sio kila ujumbe unaotumwa au unaotumiwa ni wa kweli.

Kumekuwa na usambazaji wa habari za uongo kwa kasi zaidi hasa katika kipindi hiki kigumu cha mlipuko wa Covid-19.

Watu wamekuwa wakitumiwa ujumbe wa simu ambao sio wa ukweli na wao pia kuendelea kuusambaza kwa watu tofauti.

Kutokana na jambo hili,Whatsapp imechukua hatua mpya kwa kuweka kiwango maalumu cha kutuma ujumbe kama huo.

UJumbe kama huo unaweza kutumwa mara moja tu,na sio zaidi ya hapo.

Hatua hii imechukuliwa ili kuounguza kasi ya kusambaa kwa ujumbe kama huo.

Kabla ya marufuku hii,ujumbe ulikuwa unaweza kutumwa kwa watu watano tofauti au makundi tofauti kwa wakati mmoja.Habari Zinazohusiana