Jeshi la Uturuki  lawaangamiza magaidi wa kundi la PKK

Jeshi la Uturuki lawaangamiza magaidi 14 wa kundi la PKK/YPG  katika eneo la operesheni ya Fratia

1390234
Jeshi la Uturuki  lawaangamiza magaidi wa kundi la PKK


Jeshi la Uturuki lawaangamiza magaidi 14 wa kundi la PKK/YPG  katika eneo la operesheni ya Fratia.

Magaidi 14 wa kundi la PKK waripotiwa kuangamizwa na jeshi la Uturuki katika eneo ambalo kuliendeshwa operesheni  ya Fratia dhidi ya magaidi nchini Syria.

Wizara ya ulinzi  ya Uturuki  imethibitisha vifo vya magaidi hao 14 wa kundi la PKK  baada ya kujaribu kuvamia kambi ya jeshi la Uturuki katika eneo ambalo kuliendeshwa operesheni ya  Fratia.

 Wizara ya ulinzi imeendelea kufahamisha kuwa jeshi la Uturuki litaendelea na juhudi zake za kuimarisha usalama katika ukanda.

Uturuki  imeanazisha operesheni ya Fratia mnamo Agosti  24 mwaka  2016 , Operesheni Tawi la Mzaituni Januria  20  mwaka  2018 na operesheni chanzo cha amani  Oktoba  9 mwaka  2019.
 Habari Zinazohusiana