Idadi ya maambukizi ya virusi vya corona ulimwenguni yafikia milioni 1

Watu milioni moja ulimwenguni waathirika na virusi vya corona tangu kuanza kwake  Wuhan China

1390248
Idadi ya maambukizi ya virusi vya corona ulimwenguni yafikia milioni 1


Watu milioni moja ulimwenguni waathirika na virusi vya corona tangu kuanza kwake  Wuhan China.

Idadi ya watu walioathirika na virusi vya corona ulimwenguni yaripotiwa kuongezeka na kufikia watu  milioni moja huku idadi ya watu ambao wamekwishafariki ikiripotiwa kuwa watu  51000.

Nchini Italia  idadi ya vifo bado inaripotiwa kuzidi kuongezeka,  katika kipindi cha masaa 24 watu  760 wameripotiwa kufariki.

Idadi hiyo pia imepelekea idadi ya watu waliofariki tangu kuanza kwa janga hilo imefikia watu  13915.

Ursula von der Leyen, mkurugenzi mkuu wa kamishna wa Ulaya amesema kuwa  Italia ndio  taifa mablo lilikuwa limaethirika kwa kiasi kikubwa kwa idadi ya watu wengi waliofariki kwa virusi vya corona baada ya China.

Ursula von der Leyen amesema kuwa  kulikuwa na umuhimu wa ıushirkiano katika kipindi hiki kigumu, hali haikuwa jambo rahisi kwa kuwa kila taifa tayari lilikuwa katika jango la Covid-19.

Nchini Ufaransa watu 471 wamefariki katika  kipindi cha masaa 24 na idadi ya vifo inaendelea kuongezeka na kufikia watu  4503.
Nchini Marekani  watu  5151  wamekwishafariki .


Tagi: #Covid-19

Habari Zinazohusiana