Wagonjwa wa corona kutoka Italia wapelekwa nchini Ujerumani

Baada ya ombi la msaada kutolewa na serikali ya Italia, waathirika wa Covid-19 wasafrishwa kuelekea nchini Ujerumani

1386806
Wagonjwa wa corona  kutoka Italia wapelekwa nchini Ujerumani

Wagonjwa wa corona  kutoka Italia kutibiwa Ujerumani.

Baada ya ombi la msaada kutolewa na serikali ya Italia, waathirika wa Covid-19 wasafrishwa kuelekea nchini Ujerumani.

Baada ya serikali ya Italia kutangza kuzidiwa na  janga la corona katika hospitali zake,  waathirika wa virusi hivyo wasafirishwa kuelekea nchini Ujerumani.

Wagonjwa waliokuwa katika  mji wa Bergamo wamesafrishwa na ndege ya jeshi  na kupokelewa  katika uwanja wa ndege wa jeshi wa mjini  Köln nchini Ujerumani.

Baada  ya kuwasili katika uwanja huo, waathirika hao wamepelekwa katika hospitali ya Bochum na Bonn kwa ajili ya matibabu.

Kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa,  vyumba , vitanda na vifaa vya matibabu kwa wagonjwa walio maututi vimekuwa vichache, jambo ambalo limepelekea Italia kuomba msaada  nchini Ujerumani.

Watu  10 023 wamekwishafariki nchini Italia tangu kuanza kwa virusi hivyo nchini China mwishoni mwa mwaka  2019.Habari Zinazohusiana