Shirika la Afya duniani (WHO) latoa maelezo kuhusiana na chanjo ya virusi vipya vya Corona

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Afya duniani amesema kwamba chanjo dhidi ya virusi vya cororna itapatikana ndani ya mwaka 1 au mwaka 1 na nusu

1386517
Shirika la Afya duniani (WHO) latoa maelezo kuhusiana na chanjo ya virusi vipya vya Corona

Tedros Adhanom Ghebreyesus, mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani (WHO) amesema kwamba inahitajika zaidi ya mwaka au mwaka na nusu kuweza kuja na chanjo dhidi ya virusi vipya vya Corona ( Covid-19).

Akizungumza na wanahabari kupitia mkutano na wanahabari uliofanyika kwa njia ya video, mkurugenzi mkuu wa WHO alisema, “ Inahitajika zaidi ya mwaka au mwaka mmoja na nusu kutengeneza chanjo dhidi ya Covid-19, katika kipindi hicho tunakubali kwamba suala la kuwapatia tiba wagonjwa na kuokoa maisha yao ni suala muhimu”.

 Ghebreyesus aliyekumbushia kwamba Covid-19 imeashaathiri takribani ya watu nusu milioni na kusababisha vifo vya watu zaidi ya elfu 20 alisema,

“Hio ni habari mbaya lakini duniani kwa ujumla, mamia ya watu walisalia hai na kusalimika”

Ghebreyesus, akizungumzia juu ya upungufu wa vifaa vya kujikinga hasa kwa madaktari na wahudumu wa afya alisema, “ ni tatizo la ulimwengu mzima” na “Juhudi zao za pamoja wanazozifanya katika kuokoa maisha zinawaweka kwenye matata makubwa”.

Ghebreyesus alisema kwamba wametuma zaidi ya vifaa vya kujikinga milioni 2 kwa mataifa 72 yaliyokuwa na mahitaji makubwa zaidi na pia wameshafanya maandalizi kutuma vifaa tiba kama vilivyotajwa kwa mataifa 60 zaidi.

Ghebreyesus, aliongeza kwamba ushirikiano zaidi unahitajika kwani ili kuweza kutatua changamoto hiii inahitajika mshikamano na ushirikiano wa kimataifa.

 Habari Zinazohusiana