Rais Trump ampa pole waziri mkuu wa Uingereza kwa kuambukizwa virusi vya Corona

Rais wa Marekani, Donald Trump amempa pole na kumtakia apone haraka rafiki yake waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson kufuatia hapo jana waziri mkuu huyo kutangaza amekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona

1386579
Rais Trump ampa pole waziri mkuu wa Uingereza kwa kuambukizwa virusi vya Corona

Rais wa Marekani, Donald Trump azungumza kwa njia ya simu na waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson na kumtakia apone haraka maambukizi ya virusi vipya vya Corona,Covid-19.

Taarifa iliyotolewa na ikulu ya white house imesema kwamba Rais Trump amezungumza na Johnson hii leo.

Kutokana na urafiki wao wa karibu Trump alimtakia Johnson apone haraka.

Viongozi hao 2 walikubaliana kwamba ni wakati muafaka kwa G-7, G-20 na miunganiko mingine ya kimataifa kuweka nguvu zao pamoja katika kupambana na virusi vya Corona, ili kuupa uhai upya uchumi wa dunia. Uingerza na Marekani zinamatumaini kwamba wataibuka washindi katika vita hivi na watapata nguvu zaidi ya  ilivyotokea katika milipuko iliyopita.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Johnson alituma ujumbe wa video na kusema kwamba masaa 24 yaliyopita alianza kuonyesha dalili na alipofanya vipimo ikadhihirika kwamba ana maambukizi ya virusi vya Corona.

Johnson  aliamua kujitenga mwenyewe “ kujiweka karantin” na ataendesha shughuli za serikali kutokea karantin kwa njia ya video.Habari Zinazohusiana