Jeshi la Ufaransa latangaza kuondoka nchini Irak

Kikosi cha eshi la Ufaransa kilichokuwa nchini Irak katika jeshi la ushirika dhidi ya kundi la Daesh charejea nyumbbani

1385108
Jeshi la Ufaransa latangaza kuondoka nchini Irak


Kikosi cha eshi la Ufaransa kilichokuwa nchini Irak katika jeshi la ushirika dhidi ya kundi la Daesh charejea nyumbani.

Jeshi la Ufaransa limetangaza kuondoka nchini Irak kwa kikosi chake  kilichokuwa katika jeshi la ushiriki katika mapambano dhidi ya kundi lla kigaidi la Daesh nchini humo.

Kulingana na jeshi la Ufaransa, wanajeshi wake nchini humo Irak wanaondoka kutokana na janga la virusi vya corona. 

Taarifa kuhusu jeshi la Ufaransa kuondoka nchini Irak imetolea  Jumatano Machi 25.
Kwa ushirikiano na jeshi la Irak, jeshi la  ushirikiano limechukuwa uamuzi wa kusitisha kwa muda  zoezzi la kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Irak katika  juhudi za kupamban na kundi la kigaidi la Daesh.

Jeshi la Ufaransa limefahmisha kuwa limechukua uamuzi huo  kutokana na janga la virusi vya corona, virusi ambavyo ni tishia katika pembe nne za dunia.

Wanajeshi zaidi ya  100 wa Ufaransa, kundi la kwanza litaondoka nchini humo Machi 26.

Operesheni za anga  za jeshi la Ufaransa  dhidi ya kundi la Daesh zitaendelea kutokea katika kambi yake iliopo nchini Yordania.
 Habari Zinazohusiana