"Virusi vya Corona vinaweza kuishi zaidi ya siku 17"

Wataalamu wamegundua kwamba virusi vipya vya Corona vinaweza kubaki hai katika nyuso za vitu mbalimbali hata zaidi ya siku 17

"Virusi vya Corona vinaweza kuishi zaidi ya siku 17"

Imefahamika kwamba virusi vya Corona huweza kuishi katika nyuso za vitu mara tano zaidi ya muda uliodhaniwa hapo mwanzoni. Hapo mwanzo ilidhaniwa kwamba virusi hivyo huweza kuishi kwa siku 3.

Kituo cha utafiti na udhibiti wa magonjwa nchini Marekani (CDC), kimeandaa ripoti kuhusiana na mada hiyo.Katika ripoti hiyo ilifahamishwa kwamba virusi vipya vya Corona (Covid-19) huweza kuishi katika nyuso za vitu muda mrefu zaidi kuliko ule uliodhaniwa kwa mara ya kwanza.

Katika ripoti hio ilisemwa kwamba virusi vilivyokuwa katika meli mbili zilizosafiri kutoka California na Japan, dalili zake zilionekana hata siku 17 baadae.

Kwa mujibu wa ripoti hio wataalamu walisema kwamba  walipata dalili za virusi vya Corona katika meli za abiria  ile ya  Japan, Diamond princess na ile ya California Grand Princess hata siku 17 baada ya kuwahamisha abiria kutoka katika meli hizo.


Tagi: Corona , CDC

Habari Zinazohusiana