Shirika la afya duniani (WHO) lasema huenda Marekani ikawa kitovu kipya cha mlipuko wa Corona

Kutokana na ongezeko kubwa la visa vya maambukizi ya virusi vipya vya Corona, Covid-19 shirika la afya duniani limesema huenda nchi hiyo ikawa kitovu kipya cha mlipuko wa ugonjwa huo

1384668
Shirika la afya duniani (WHO) lasema huenda Marekani ikawa kitovu kipya cha mlipuko wa Corona

Margaret Harris, msemaji wa shirika la afya duniani,WHO, amesema kwamba huwenda Marekani ikawa kitovu kipya cha mlipuko wa virusi vipya vya Corona (Covid-19).

Msemaji huyo wa WHO alitanabaisha kwamba katika masaa 24 yaliyopita visa vya maambukizi yz virusi vipya vya Corona nchini Marekani na Ulaya ni asilimia 85 ya visa vyote duniani na huwenda Marekani ikawa kitovu kipya cha mlipuko wa virusi.

Katika taarifa aliyoitoa Haris kupitia mkutano na wanahabari uliofanyika kwa njia ya video alisema kwamba idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa virusi vipya vya Corona itaongezeka kwa kiasi kikubwa.

Harris aliongeza kwamba mlipuko huo utaendelea kuenea kwa kasi.

“ Ilichukua miaka 2 kwa mlipuko mbaya kabisa wa Ebola uliotokea Afrika magharibi kusababisha vifo vya watu elfu 11, ni kwa ajili hiyo tunasema kwamba hivi sasa tunakabaliana na mlipuko mbaya zaidi”.

Harris alisisitiza kwamba Ulaya na Marekani ni katika maeneo ambayo yameathirika zaidi na mlipuko wa virusi.

“Baadhi ya mataifa yamepiga marufuku kutoka nje na kuweka karantin wagonjwa, hatua hizi zinapunguza kuenea kwa ugonjwa na  pia zinasaidia vituo vya afya na wafanyakazi wa afya kupata muda wa kutosha kupanda na mlipuko” alisema Harris

Harris alipoulizwa kama Marekani inaweza kuwaa kitovu kipya cha mlipuko alisema,

“Ukiangalia visa vya maambukizi nchini Marekani utagundua kwamba kuna ongezeko kubwa mno. Kwa hiyo uwezekano huo upo”.

Mnamo Machi 13, mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani, Tedros Adhanom Ghebreyesus, alisema kwamba bara la Ulaya limekuwa kiini kipya cha maambukizi ya Kovid-19.

 


Tagi: #Covid-19 , #WHO

Habari Zinazohusiana